Wednesday, July 23, 2014

MARI WAFANYA UKAGUZI WA MIRADI INAYOFANYWA MKOANI TANGA WILAYANI MUHEZA.

Kituo cha utafiti wa mazao ya kilimo kilichopo mikocheni jijini Dar es salaam, kilifanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali iliyopo chini ya kituo hicho, katika ziara hiyo miradi iliyokaguliwa ni pamoja na mradi wa mahindi yanayovumilia ukame, mradi ulio chini ya usimamizi wa Dr. Ruth Maduru, na mwingine ni ule mradi wa matunda aina ya maembe na michungwa na upo chini ya usimamizi wa Dr. Christopher Materu. Miradi hii inafadhiliwa na Tume ya sayansi na teknolojia.
Wafanyakazi wa MARI wakiwa katika picha ya pamoja katika hifadhi ya Taifa ya amani - Tanga.

Huu ni mmoja kati ya miti ya michungwa iliyo katika majaribio ya kuzuia wadudu
Mti wa muembe ulioshambuliwa na viwavi
Watafiti kutoka MARI katika shamba la michungwa wilayani - Muheza Tanga
Mama Beatrice Mruma (kati) akiwaeleza watafiti kutoka MARI njia mbalimbali za kuua wadudu
Watafiti kutoka MARI wakiangalia mahindi yanayovumilia ukame

No comments:

Post a Comment