Friday, July 25, 2014

MARI YATOA MAFUNZO KWA MAAFISA UGANI KUTOKA SEKTA YA CHAI.

Kituo cha utafiti wa mazao ya kilimo cha mikocheni, kimetoa mafunzo kwa maafisa ugani katika sekta ndogo ya chai, kutoka taasisi mbalimbali hapa nchini kama vile wakala wa wa maendeleo ya wakulima wadogo, bodi ya chai, taasisi ya utafiti wa chai na baadhi ya halmashauri zinazolima chai hapa Tanzania.Dhumuni la mafunzo haya ni kuwafundisha maafisa ugani jinsi ya kuzalisha chai kwa wingi kwa kutumia njia ya chupa (tissue culture). Mafunzo hayo yalianza tarehe 24 July mpaka 25 July, 2014.
Washiriki wakipiga picha ya Pamoja na Afisa mfawidhi wa kituo cha MARI, Dr. Joseph Ndunguru
Hamza msangi akiwaonesha washiriki jinsi ya kuzalisha mimea kwa kutumia chupa
Dr. Fred Tairo akiwaeleza washiriki wa mafunzo hayo jinsi ya kupata vina saba kutoka kwenye sampuli za majani ya mihogo
Dr. Fred Tairo akiwaelezea washiriki kazi mbalimbali zifanywazo kwenye maabara ya (molecular laboratory).
Washiriki wakimsikiliza mkufunzi
Washiriki wakimsikiliza mratibu wa mradi wa chai Dr. Joseph Ndunguru.

No comments:

Post a Comment