Monday, August 4, 2014

MARI YASHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE MKOANI MOROGORO.

Ikiwa ni maonesho ya 22 ya nane nane (maonesho ya kilimo), kituo cha utafiti wa mazao ya kilimo cha mikocheni kimepata fursa ya kuhudhuria maonesho hayo, ili kuonesha teknolojia mbalimbali zinazofanywa na kituo hicho, ikiwemo teknolojia ya uzalishaji mimea kwa kutumia chupa. Kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu ni " Matokea makubwa sasa" Kilimo ni biashara
Hamza Msangi akiwaelezea wanafunzi jinsi ya kuotesha mimea kwa njia ya chupa
Veronica Kibambi akiwaonesha wakulima jinsi ya kutumia kifaa maalumu kwa ajili ya kukunia nazi.
Banda la Utafiti na maendeleo kanda ya mashariki
Joyce challe akimueleza mkulima jinsi ya kutumia mafuta ya mwali yatokanayo na zao la nazi
Happiness Gabriel akimuonesha mkulima jinsi ya kuotesha mimea kwa kutumia chupa.
Dr. Christopher Materu akimuonesha mkulima mtego kwa ajili ya kutega nzi wavamizi wa matunda.

1 comment: