Wakulima waliopata utaalamu wa kuzuia wadudu wanaoshambulia matunda kutoka Muheza - Tanga kupitia kituo cha utafiti wa mazao ya kilimo cha mikocheni (MARI) walipata fursa ya kutembelea banda la utafiti na maendeleo ili kujionea tafiti mbalimbali zinazofanywa na Idara ya utafiti na maendeleo iliyo chini ya wizara ya kilimo chakula na ushirika.
Wednesday, August 6, 2014
Monday, August 4, 2014
MARI YASHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE MKOANI MOROGORO.
Ikiwa ni maonesho ya 22 ya nane nane (maonesho ya kilimo), kituo cha utafiti wa mazao ya kilimo cha mikocheni kimepata fursa ya kuhudhuria maonesho hayo, ili kuonesha teknolojia mbalimbali zinazofanywa na kituo hicho, ikiwemo teknolojia ya uzalishaji mimea kwa kutumia chupa. Kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu ni " Matokea makubwa sasa" Kilimo ni biashara
Hamza Msangi akiwaelezea wanafunzi jinsi ya kuotesha mimea kwa njia ya chupa |
Veronica Kibambi akiwaonesha wakulima jinsi ya kutumia kifaa maalumu kwa ajili ya kukunia nazi. |
Banda la Utafiti na maendeleo kanda ya mashariki |
Joyce challe akimueleza mkulima jinsi ya kutumia mafuta ya mwali yatokanayo na zao la nazi |
Happiness Gabriel akimuonesha mkulima jinsi ya kuotesha mimea kwa kutumia chupa. |
Dr. Christopher Materu akimuonesha mkulima mtego kwa ajili ya kutega nzi wavamizi wa matunda. |
Friday, July 25, 2014
MARI YATOA MAFUNZO KWA MAAFISA UGANI KUTOKA SEKTA YA CHAI.
Kituo cha utafiti wa mazao ya kilimo cha mikocheni, kimetoa mafunzo kwa maafisa ugani katika sekta ndogo ya chai, kutoka taasisi mbalimbali hapa nchini kama vile wakala wa wa maendeleo ya wakulima wadogo, bodi ya chai, taasisi ya utafiti wa chai na baadhi ya halmashauri zinazolima chai hapa Tanzania.Dhumuni la mafunzo haya ni kuwafundisha maafisa ugani jinsi ya kuzalisha chai kwa wingi kwa kutumia njia ya chupa (tissue culture). Mafunzo hayo yalianza tarehe 24 July mpaka 25 July, 2014.
Washiriki wakipiga picha ya Pamoja na Afisa mfawidhi wa kituo cha MARI, Dr. Joseph Ndunguru |
Hamza msangi akiwaonesha washiriki jinsi ya kuzalisha mimea kwa kutumia chupa |
Dr. Fred Tairo akiwaeleza washiriki wa mafunzo hayo jinsi ya kupata vina saba kutoka kwenye sampuli za majani ya mihogo |
Dr. Fred Tairo akiwaelezea washiriki kazi mbalimbali zifanywazo kwenye maabara ya (molecular laboratory). |
Washiriki wakimsikiliza mkufunzi |
Washiriki wakimsikiliza mratibu wa mradi wa chai Dr. Joseph Ndunguru. |
Wednesday, July 23, 2014
MARI WAFANYA UKAGUZI WA MIRADI INAYOFANYWA MKOANI TANGA WILAYANI MUHEZA.
Kituo cha utafiti wa mazao ya kilimo kilichopo mikocheni jijini Dar es salaam, kilifanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali iliyopo chini ya kituo hicho, katika ziara hiyo miradi iliyokaguliwa ni pamoja na mradi wa mahindi yanayovumilia ukame, mradi ulio chini ya usimamizi wa Dr. Ruth Maduru, na mwingine ni ule mradi wa matunda aina ya maembe na michungwa na upo chini ya usimamizi wa Dr. Christopher Materu. Miradi hii inafadhiliwa na Tume ya sayansi na teknolojia.
Wafanyakazi wa MARI wakiwa katika picha ya pamoja katika hifadhi ya Taifa ya amani - Tanga. |
Huu ni mmoja kati ya miti ya michungwa iliyo katika majaribio ya kuzuia wadudu |
Mti wa muembe ulioshambuliwa na viwavi |
Watafiti kutoka MARI katika shamba la michungwa wilayani - Muheza Tanga |
Mama Beatrice Mruma (kati) akiwaeleza watafiti kutoka MARI njia mbalimbali za kuua wadudu |
Watafiti kutoka MARI wakiangalia mahindi yanayovumilia ukame |
Subscribe to:
Posts (Atom)